Merci Henock Inonga

Klabu yetu imefikia makubaliano ya kumuuza mlinzi wa kati, Henock Inonga Baka kwenda FA Rabat inayoshiriki Ligi Kuu nchini Morocco.

Inonga raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amebakisha Mkataba wa mwaka mmoja unaomalizika 2025 lakini kutokana na klabu yetu kujali na maslahi ya wachezaji, tumemruhusu beki huyo kuondoka kwenda kujiunga na FA Rabat.

Inonga alijiunga na kikosi chetu mwaka 2021 akitokea  DC Motema Pembe ya Congo.

Katika kipindi cha miaka mitatu alichodumu ndani ya kikosi chetu Inonga amekuwa muhimili wa timu na makocha wote waliopita wamekuwa wakimpa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Mwaka 2022 Inonga alichaguliwa mlinzi bora wa Ligi kuu ya Tanzania baada ya kuonesha kiwango bora katika msimu huo.

Uongozi unamshukuru Inonga kwa utumishi wake uliotukuka katika kipindi chote tulichokuwanae na pia tunamtakia kheri katika maisha yake mapya ya soka nje ya Simba.

Kuondoka kwa Inonga ni muendelezo wa maboresho makubwa yanayoendelea ndani ya kikosi chetu

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER