Meneja afunguka kuhusu Inonga na Timu ya Taifa ya Congo

Meneja Patrick Rweyemamu ameweka wazi kuwa klabu ilitumiwa taarifa kuhusu kuitwa kwenye kikosi cha awali cha Timu ya Taifa ya DR Congo mlinzi Henock Inonga Baka kinachojiandaa na mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Madagascar.

Rweyemamu amesema klabu imetumiwa barua rasmi na DR Congo kuhusu kuitwa Inonga na ndio sababu jina lake likajumuishwa kwenye wachezaji wetu 16 walioitwa timu zao za taifa.

Meneja Rweyemamu ameongeza kuwa lakini katika kikosi cha mwisho kitakachoivaa Madagascar jina lake limeenguliwa na ndiyo maana yupo mazoezini na wenzake akijifua.

“Tulipokea barua kutoka timu ya Taifa ya DR Congo inayojiandaa na mchezo dhidi ya Madagascar kumtaka mlinzi wetu Henock Inonga kujiunga nayo katika kikosi cha awali lakini baada ya mchujo amewekwa pembeni kusubiri kama atahitajika,” amesema Rweyemamu.

Katika taarifa yetu tuliyoitoa tumeorodhesha jina la Inonga miongoni mwa wachezaji wetu 16 walioitwa timu zao za taifa na tulikuwa sahihi sababu tumepokea barua rasmi kutoka DR Congo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER