Mels Daalder Skauti Mkuu Simba

Uongozi wa klabu umemteua Mels Daalder Raia wa Uholanzi kuwa msaka vipaji (Skauti Mkuu) ambaye ana uzoefu wa kufanya skauti kwenye timu mbalimbali.

Mels ameshiriki kozi mbalimbali za duniani ikiwa ni pamoja na zilizoendeshwa na skauti wa zamani wa Manchester United, David Hobson.

Mels ambaye ameshawahi kuishi Tanzania ni shabiki mkubwa wa Simba pia ni mjuzi wa kufanya upembuzi (analysis) na anaijua vizuri ligi ya Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

Mels anaongea lugha kadhaa ikiwemo Kiholanzi, Kiingereza, Kijerumani, Kifaransa na Kiswahili kwa kiasi fulani.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu, Imani Kajula amesema eneo la skauti ni muhimu ingawa lilikuwa haipewi nafasi kubwa na kwa kuliona hilo tumeamua kumleta Mels.

” Tunafuraha kubwa kumkaribisha Mels ili kuja kuboresha ufanisi kwenye skauti kwakuwa ni eneo muhimu katika mafanikio ya klabu yetu. Tunaendelea na maboresho muhimu kuelekea msimu mpya wa ligi na mashindano ya kimataifa,” amesema Kajula.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER