Bodi ya Ligi (TPLB) imehairisha baadhi ya mechi zetu ili kupisha mchezo kati ya timu ya taifa ya Zanzibar Heroes na Tanzania Bara ambayo itatumika kufungua uwanja wa Amaan, Zanzibar ambao umefanyiwa ukarabati mkubwa.
Hii ina maanisha mechi zetu nne ambazo tulitakiwa kuzicheza kuanzia Disemba 26 hadi Januari tano kuahirishwa.
Mechi zetu zilizoahirishwa ni
Disemba 26, Mashujaa vs Simba
Disemba 29, Tabora United vs Simba
Januari Mosi, Azam vs Simba
Januari 4, Geita Gold vs Simba