Mechi yetu dhidi ya Ihefu kupigwa kesho saa moja usiku Chamazi

Mchezo wetu wa Robo Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Ihefu FC utafanyika kesho saa moja usiku katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Awali mchezo huo ulipangwa na kutangazwa kuwa utafanyika saa 10 jioni katika dimba hilo hilo la Azam Complex lakini muda huo umebadilishwa sasa utapigwa usiku.

Maamuzi ya kusogeza muda mbele ni kuwapa nafasi mashabiki waliopo kwenye Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kufuturu na wale Wakristo kufanya ibada ya Ijumaa Kuu.

Mchezo huo utakuwa ni wa kwanza kwetu kucheza katika Uwanja wa Azam Complex msimu huu kufuatia ukarabati unaoendelea katika Uwanja wa Benjamin Mkapa tunaotumia kwa mechi za nyumbani.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER