Mchezo wetu wa Ngao ya Jamii kupigwa Agosti 10 Mkwakwani

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeweka hadharani ratiba ya mchezo wetu wa Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Fountain Gate FC kuwa utapigwa Agosti 10 katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga saa moja usiku.

TFF imefanya mabadiliko ya kanuni kwenye mechi za Ngao ya Jamii ambapo msimu huu itashirikisha timu nne na si mbili kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Mshindi wa mchezo wetu atakutana na atakayeibuka kidedea kwenye mechi ya Yanga dhidi ya Azam FC.

Atakayepoteza nae atakutana na atakeshindwa katika mchezo wa Yanga dhidi ya Azam.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER