Mchezo wetu dhidi ya JKT Tanzania kupigwa Isamuhyo Alhamisi

Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya JKT Tanzania utapigwa katika Uwanja wa Meja Jenerali Michael Isamuhyo Alhamisi saa 10 jioni.

Baada ya kikosi kurejea jana usiku kutoka jijini Mwanza wachezaji walipewa mapumziko na kesho watafanya mazoezi kujiandaa na mchezo huo.

Utakuwa mchezo mgumu kutokana na nafasi waliyopo wenyeji JKT hasa ukizingatia wanacheza katika Uwanja wao wa nyumbani lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

Malengo ya timu ni kupambana kupata ushindi kwenye kila mchezo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER