Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji uliopangwa kufanyika Alhamisi, Mei 16 katika Uwanja wa Jamhuri umesogezwa mbele kwa siku moja sasa utachezwa siku ya Ijumaa.
Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi imesema mchezo huo umesogezwa mbele siku moja ili kuipa nafasi ya kikanuni Dodoma Jiji ya kucheza mechi baada ya saa 72.
Maandalizi ya mchezo huo yanaendelea na leo asubuhi kikosi kimefanya mazoezi ya utimamu wa mwili katika Uwanja wa Kaitaba kabla ya kuanza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam.