Mchezo wetu dhidi ya Coastal kupigwa Septemba 21

Mchezo wetu wa Ligi ya NBC ambao ulikuwa haujapangiwa tarehe dhidi ya Coastal Union sasa utapigwa Septemba 21 katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam saa 10 jioni.

Mchezo huo ulikuwa haupangiwa tarehe kutokana na ratiba ya ushiriki wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na mechi za kufuzu michuano ya Afrika (AFCON).

Baada ya mchezo wetu wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos ya Zambia utakaopigwa Septemba 16 kikosi kitarejea jijini Dar es Salaam kujiandaa na mechi ya Coastal.

Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) imeweka wazi kuwa mchezo wetu dhidi ya Tanzania Prisons ambao ulipangwa kupigwa Oktoba 3, katika Uwanja wa Sokoine umesogezwa mbele hadi Oktoba 5, kwakuwa mechi yetu ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos itachezwa Oktoba Mosi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER