Mchezo dhidi ya Singida Black kupigwa Disemba 28

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya maboresho ya ratiba ya Ligi na kuzipangia ratiba mechi mbalimbali ambazo zilikuwa hazijapangiwa kutokana na sababu tofauti.

Mchezo namba 100 wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Black Stars ambao awali ulikuwa haujapangiwa tarehe sasa utapigwa Disemba 28 saa 10 jioni katika Uwanja wa Liti.

Kupangwa mchezo huo kunaondoa mechi yetu dhidi ya Tabora United ambayo ilipangwa kuchezwa tarehe hiyo.

Marekebisho hayo yatafanya timu zote kucheza mechi sawa na zitakamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi.

Mechi zetu zilizosalia kukamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi ni hizi:

Simba vs Ken Gold (Disemba 18)

Kagera Sugar vs Simba (Disemba 21)

Simba vs JKT Tanzania (Disemba 24)

Singida Black Stars vs Simba (Disemba 28)

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER