Mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy kupigwa Fransictown

Mchezo wetu wa pili wa hatua ya makundi wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy utachezwa katika Mji wa Fransictown baadala ya Mji wa Gaborone kama ilivyozoeleka.

Sababu za mchezo huo kuhamishwa ni kutokana na Uwanja wa Taifa wa Botswana kufungiwa.

Kwa sasa mchezo wetu dhidi ya Galaxy utachezwa katika Uwanja Obedi Itani Chilume uliopo katika Mji huo wa Francistown ambao ni kilometa 450 kutoka Gaborone.

Uwanja wa Obedi Itani zamani ukifahamika kama Francistown Sports Complex ndo uwanja mkubwa nchini Botswana wenye uwezo wa kuingiza mashabiki Elfu 26.

Kwa sasa kikosi chetu kinaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo huo ambao tunahitaji kupata pointi tatu ili kujiweka kwenye nafasi nzuri katika kundi letu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER