Mazoezi ya mwisho kabla ya kuivaa Mtibwa kesho

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa saa moja usiku katika dimba la Benjamin Mkapa.

Wachezaji wote waliocheza mechi yetu ya mwisho dhidi ya Azam FC wameshiriki mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo wa huo.

Morali ya wachezaji ipo juu na kila mmoja amefanya jitihada mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi kesho.

Pointi tatu katika mchezo wa kesho ni muhimu kwetu kwakuwa tunahitaji kurudisha hali ya kujiamini kwa wachezaji mpaka mashabiki.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER