Mazembe kutua Kesho

Kikosi cha wachezaji 23 wa TP Mazembe pamoja na benchi la ufundi watatua kesho saa saba mchana tayari kwa mchezo wa kirafiki katika kilele cha tamasha la Simba Day Jumapili.

Mabingwa hao mara tano wa Ligi ya Mabingwa Afrika watakuja na ndege ya Shirika la Ethiopian Air Line wakiwa na kikosi chao kamili.

Tumeamua kuichagua Mazembe kwa kuwa tunaamini itatupa mechi nzuri na itakuwa burudani kwa mashabiki watakaojitokeza katika Tamasha la Simba Day.

Ukiacha mchezo huo kirafiki siku hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka wasanii na shamra shamra kuanzia saa tatu asubuhi

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER