Kocha Msaidizi Seleman Matola amewaita mashabiki kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Liti kesho kwa ajili ya kuisapoti timu kwenye mchezo wa kesho wa Ligi kuu ya NBC dhidi ya Ihefu FC.
Matola amewaomba radhi mashabiki kutokana na kushindwa kufanya vizuri kwenye mechi zetu zilizopita lakini kwa kesho tupo tayari kuhakikisha tunawapatia furaha.
Matola ameongeza kuwa kikosi kimepata siku mbili ya kufanya mazoezi mkoani Singida na wachezaji wapo kwenye hali nzuri na tumejipanga vizuri kwa ajili ya kupata ushindi.
“Tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kesho, tunajua wameumizwa na matokeo yetu ya mechi zetu zilizopita lakini tumejipanga, tunawaahidi tutawapa furaha,” amesema Matola.
Kwa upande wake nahodha msaidizi Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema wachezaji wapo tayari kupambana na kila mmoja yupo kamili.
“Sisi kama wachezaji tupo tayari kwa ajili ya kupata ushindi kwenye mchezo wa kesho, tunajua itakuwa mechi ngumu lakini tumejiandaa vya kutosha,” amesema Zimbwe Jr.