Matola: Tunashukuru tumemaliza msimu salama

Kaimu Kocha Mkuu Seleman Matola, amesema baada ya kumalizika rasmi kwa msimu wa ligi 2021/22 salama sasa tunajipanga kwa maandalizi ya msimu ujao.

Matola amesema hatukuwa na msimu mzuri lakini imekuwa funzo kwetu na tutahakikisha tunarejesha kila tulichopoteza.

Akiuzungumzia mchezo wa leo dhidi ya Mbeya Kwanza, Matola amesema ulikuwa mzuri kutokana na timu zote kucheza bila presha.

Matola ameongeza kuwa kila timu ilijitahidi kuonyesha umahiri na ufundi mkubwa kwa kuwa hakukuwa na chakupoteza.

“Msimu umeisha salama na hilo ni jambo la kushukuru Mungu kikubwa ni kujipanga kwa ajili ya msimu ujao turudi kwa nguvu.

“Mchezo wa leo ulikuwa mzuri kila timu ilicheza kwa mipango na kuonyesha ufundi kwa kuwa hakukuwa na presha,” amesema Matola.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER