Matola: Tulitegemea mechi dhidi ya Singida ingekuwa ngumu

Kocha Msaidizi wa timu yetu, Seleman Matola amesema tulitegemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Singida Fountain Gate katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi.

Matola amesema Singida wana timu nzuri inayoundwa na wachezaji wenye vipaji na uzoefu ndio maana tulitegemea kupata upinzani mkubwa.

Matola ameongeza kuwa Singida walikuwa bora katika dakika 25 za mwanzo za kipindi cha kwanza na ndipo walipopata bao la kuongoza lakini cha pili walirudi nyuma na kutuacha tutawale sehemu kubwa.

“Kabla ya mchezo nilisema haitakuwa mechi rahisi kutokana na ubora wa wapinzani wetu, lakini nawapongeza wachezaji wangu kwa jitihada kubwa walizofanya licha ya kuwa nyuma kwa muda mrefu.”

“Ilikuwa mechi ngumu sasa tuna siku mbili za kujiandaa na mchezo wa fainali dhidi ya Mlandege,” amesema Matola.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER