Kocha Msaidizi Seleman Matola, amesema tulikuwa bora kwenye mchezo wa leo dhidi ya Tanzania Prisons na tulistahili kupata ushindi.
Matola amesema Prisons walicheza mchezo wa kuzuia zaidi katika eneo lao na kuwafanya kuwa wengi hivyo ikawa ngumu kwetu kuwapita hasa kipindi cha kwanza.
Amesema katika kipindi cha pili tulijaribu kuwafungua na kutengeneza nafasi nyingi ikiwemo penati iliyotupatia bao la ushindi.
“Tulikuwa bora zaidi yao, tulitengeneza nafasi lakini hatukuzitumia vizuri. Tulivyorudi kipindi cha pili tulikuwa imara na kufanikiwa kupata ushindi muhimu.
“Ushindi wa leo utarudisha morali na hali ya kujiamini kwa wachezaji kutokana kupitia kipindi kigumu katika mechi zetu tatu zilizopita,” amesema Matola.
One Response