Matola: Tulistahili ushindi mnono zaidi dhidi ya Mbeya Kwanza

Kocha Msaidizi Seleman Matola, amesema katika mchezo wa jana wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mbeya Kwanza tulikuwa na uwezo wa kupata ushindi mnono zaidi kama tungeongeza umakini.

Matola amesema kipindi cha kwanza tulipoteza nafasi za wazi ambazo kama tungezitumia vizuri tungeenda mapumziko tukiwa mbele kwa mabao mawili au matatu.

Hata hivyo, Matola amesema anashukuru kwa kupata pointi tatu muhimu ambazo zimezidi kupunguza tofauti na walio juu yetu.

“Tulicheza vizuri vipindi vyote viwili, tulitengeneza nafasi na kumiliki mpira. Kama tungeongeza umakini tungeshinda zaidi ya bao moja. Tunamshukuru Mungu kwa hili pia tunajipanga kwa mechi inayofuata,” amesema Matola.

Akizungumzia mchezo unaofuata wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas, Matola amesema tuna muda wa siku sita kuwaandaa kisaikolojia wachezaji na mazoezi ili tupate ushindi nyumbani.

“Tunarudi mazoezini kujiandaa na mchezo huo, tuna siku sita za kufanya mazoezi na kuwaandaa wachezaji kimwili na kiakili. Ni mchezo mkubwa na tunapaswa kushinda tukiwa nyumbani,” amesema Matola.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER