Matola: Tuko tayari dhidi ya Prisons

Kocha Msaidizi Seleman Matola, amesema maandalizi kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku yamekamilika na kila kitu kiko sawa.

Matola amesema mchezo utakuwa mgumu kutokana na nafasi iliyopo Prisons kwenye msimamo lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

Pamoja na ugumu uliopo Matola amesema timu itakayokuwa bora ndani ya dakika 90 ndiyo itaibuka na ushindi na maandalizi tuliyofanya anaamini tutachukua alama zote tatu.

“Tanzania Prisons ni timu nzuri na inacheza soka la nguvu ingawa inashika nafasi ya mwisho kwenye msimamo lakini haimaanishi kuwa itakuwa mechi nyepesi kwetu. Tumejipanga kuwakabili na hatimaye tuchukue alama zote tatu.

“Jonas Mkude ameanza mazoezi jana kwa hiyo hatakuwa tayari kwa mchezo wa kesho, Kibu Denis bado anaendelea kuuguza jeraha,” amesema Matola.

Kwa upande wake Gadiel Michael amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na morali ipo juu na amewaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi huku akiahidi kuwapa furaha.

“Sisi kama wachezaji tupo tayari kupambana kuhakikisha tunashinda mchezo wa kesho. Tunaiheshimu Prisons lakini tunahitaji kupata alama zote tatu,” amesema Gadiel.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER