Matola: Simba ya msimu ijayo tishio

Kocha Msaidizi Seleman Matola, ameupongeza uongozi pamoja na Kamati ya Usajili kwa kufanya usajili ambao umeziba mapungufu yote yaliyokuwepo msimu uliopita.

Matola amesema kwa sasa kila namba kikosini ina wachezaji bora zaidi ya mmoja hivyo imeongeza ushindani mkubwa mazoezini kila mmoja anajitahidi kulishawishi benchi la ufundi.

Matola pia ameupongeza uongozi kwa kumleta Kocha Zoran Maki ambaye falsafa zake zinaendana na timu hivyo imekuwa rahisi wachezaji kuelewa anachofundisha.

“Leo ni siku ya 11 tangu tulivyoanza kambi yetu hapa Misri, jambo zuri ni kwamba imekuwa rahisi kwa wachezaji kuelewa mafunzo ya kocha na hii inatoka falsafa yake inaendana na timu.

“Niupongeze uongozi kwa kufanya usajili mzuri pamoja na kumleta kocha Zoran. Mimi niwahakikishie msimu ujao tutakuwa na timu imara ambayo kila Mwanasimba ataifurahia,” amesema Matola.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER