Matola: Robo tatu ya wachezaji wanaumwa

Kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC, Kocha Msaidizi Seleman Matola amesema asilimia kubwa ya wachezaji pamoja na benchi la ufundi lililosafiri kuja Kagera wanaugua mafua na kifua.

Amesema wachezaji wetu wanaosumbuliwa ugonjwa huo wamekabidhiwa kwa jopo la madaktari ambao wanaendelea kuchukua vipimo ili kujua tatizo

Matola amesema inawezekana ni kutokana na hali ya hewa lakini tunasubiri vipimo vya madaktari ili kujua ukubwa wa tatizo.

“Tumefika salama jana hapa Kagera lakini changamoto kubwa tuliyokutana nayo ni kwamba robo tatu ya wachezaji wetu wanaumwa mafua, kifua na homa.

“Mimi mwenyewe nimeamka mafua yamenibana nimekuja tu hapa kwenye mkutano na waandishi lakini sipo vizuri kiafya, kwa hiyo tutaangalia hali itakavyokuwa,” amesema Matola.

Kuhusu mchezo wa kesho Matola amesema utakuwa mgumu na siku zote kila timu inapokutana nasi lazima ikaze kwa kuwa sisi ni mabingwa lakini tupo tayari kuwakabili.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER