MATOLA: NI MECHI, TUMEJIPANGA KUSHINDA

Kocha Msaidizi, Seleman Matola amesema mchezo wa kesho wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly utakuwa mgumu lakini wamejiandaa kuhakikisha wanapata alama zote nyumbani.

Matola amesema timu zote zilizopo kwenye michuano hiyo ni bora ndiyo maana ikaitwa Ligi ya Mabingwa.

Kuhusu hali ya kikosi nahodha huyu wa zamani amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na hakuna atakayekosekana kutokana kwa sababu zozote ikiwamo majeruhi.

“Mchezo utakuwa mgumu, Al Ahly ni timu kubwa yenye historia kubwa barani Afrika lakini sisi tupo nyumbani na tumejipanga kuhakikisha tunatumia vyema uwanja wa nyumbani kwa kupata ushindi.

“Wachezaji wote wako vizurii na jambo jema ni kwamba hakuna majeruhi yeyote hivyo tutaangalia jinsi watakavyomka ili tupange kikosi,” amesema Matola.

Katika mechi hiyo, tutaingia tukiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao moja tulilopata ugenini dhidi ya AS Vita wiki mbili zilizopita.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER