Matola: Mchezo dhidi ya Mtibwa utakuwa mgumu

Kaimu Kocha Mkuu Seleman Matola, amebainisha kuwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mtibwa Sugar utakuwa mgumu kutokana na ‘wakata miwa’ hao kutokuwa kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa ligi.

Amesema mara zote ligi inapoelekea ukingoni mechi zinakuwa ngumu kutokana na kila timu kutaka kumaliza vizuri msimu.

Matola amesema kikosi kipo kwenye hali nzuri, morali ya wachezaji ipo juu na tunasisitiza tunahitaji kushinda katika kila mchezo.

Kiungo huyo wa zamani ameongeza kuwa amepanga kuendelea kuwapa nafasi wachezaji ambao hawakutumika sana msimu huu huku akikiri majeruhi wanaendelea kutusumbua.

“Mchezo utakuwa mgumu, Mtibwa ni timu nzuri na haipo katika nafasi nzuri hivyo watataka kuhakikisha wanapata pointi tatu lakini tupo tayari kuwakabili.

“Wachezaji wetu wapo kwenye hali nzuri na bado tunahitaji kuhakikisha tunashinda katika mchezo wetu uliobaki,” amesema Matola.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER