Matola: Maandalizi dhidi ya Dodoma yamekamilika

Kocha Msaidizi Seleman Matola, amesema maandalizi ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigiwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku yamekamilika.

Matola amesema baada ya timu kurejea kutoka Zanzibar kikosi kimepata nafasi ya kufanya mazoezi siku mbili na wachezaji wapo kwenye hali nzuri.

Matola ameongeza kuwa katika mchezo wa kesho tutamkosa Shomari Kapombe na Peter Banda ambao ni majeruhi huku Pape Sakho akikosekana pia kutokana na kupata msiba.

Kuhusu mchezo wenyewe Matola amesema utakuwa mgumu ingawa Dodoma hawajaanza vizuri msimu lakini haitakuwa rahisi hivyo tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi.

“Tumepata muda wa siku mbili kufanya mazoezi baada ya kurudi Zanzibar, tunajua utakuwa mchezo mgumu licha ya Dodoma kuanza vibaya ligi lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

“Tutawakosa Kapombe na Banda ambao ni majeruhi wakati Sakho amepata matatizo ya kifamilia amefiwa na ndugu yake hivyo naye hatakuwa sehemu ya mchezo,” amesema Matola.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER