Matola: Ligi ni ngumu lakini tupo tayari kwa Mashujaa Kesho

Kocha Msaidizi, Seleman Matola amesema wakati ligi ikiwa imeingia mzunguko wa pili kila timu inajipanga kuhakikisha inakusanya pointi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri zaidi.

Matola ameyasema hayo mbele ya Waandishi wa Habari wakati akizungumzia maandalizi ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mashujaa FC utakaopigwa saa 2:15 usiku katika Uwanja wa Azam Complex.

Matola amesema Mashujaa haikuanza vizuri msimu lakini sasa wapo kwenye kiwango bora na anategemea kupata upinzani mkubwa lakini tumejipanga kuwakabili.

“Ligi inaelekea ukingoni, kila timu inataka kuondoka nafasi iliyopo kujiweka sehemu nzuri zaidi. Tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Mashujaa lakini tumejipanga,” amesema Matola.

Kwa upande wake mlinzi wa kulia, Israel Patrick amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri na wapo tayari kuhakikisha pointi tatu zinapatikana kesho.

“Kwa upande wetu wachezaji tupo tayari kupambana kuhakikisha tunapata pointi tatu katika mchezo wa kesho,” amesema Israel.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER