Matola: Kutopata matokeo hakujatuvunja moyo

Kocha Msaidizi Seleman Matola, amesema kikosi chetu kipo tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi Ruvu Shooting utakaopigwa Uwanja kwa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Matola amesema baada ya kurudi kutoka mkoani Lindi katika mchezo dhidi ya Namungo kikosi kiliingia kambini moja kwa moja tayari kwa mtanange huo.

Matola amesema hatujapata ushindi katika michezo mitatu iliyopata lakini jambo hilo halijashusha morali yetu na tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi.

“Tunajua mchezo utakuwa mgumu, Ruvu ni timu nzuri na ipo kwenye nafasi mbaya katika msimamo hivyo wanahitaji ushindi ili kujinasua lakini tupo tayari kuwakabili.

“Kikosi kipo kwenye hali nzuri wachezaji wote wapo tayari isipokuwa Hassan Dilunga na Sadio Kanoute ambao ni majeruhi,” amesema Matola.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER