Matola: Hatutaichukulia poa Geita

Kuelekea mchezo wetu wa kesho dhidi ya Geita Gold, Kocha Msaidizi Seleman Matola amesema hatutawadharau wapinzani hao badala yake tutaingia uwanjani kamili kutafuta alama tatu muhimu.

Matola amesema Geita si timu mbaya inacheza kitimu na tumechukua tahadhari zote kabla ya kushuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kesho kuwakabili.

Matola amesema kitu kizuri ni kwamba wachezaji wote wapo kambini tayari kwa mchezo huo hivyo benchi la ufundi litaamua nani aanze.

“Geita si timu mbaya, iko vizuri na tunaiheshimu. Tutaingia katika mchezo wa kesho tukiwa na tahadhari zote tunahitaji kupata alama zote tatu. Wachezaji wote wapo kambini tayari kwa mchezo wa kesho,” amesema Matola.

Matola amesema kwa kuwa tunaelekea katika mechi mbili kubwa ya marudiano dhidi ya Red Arrows na Yanga kwenye ligi kuu tunataraji kufanya mabadiliko kidogo ya kikosi kitakachoshuka dimbani kesho.

“Kuna mechi mbili kubwa zipo mbele yetu na wachezaji wote wamerudi kikosini kwa hiyo tunategemea kufanya mabadiliko ya kikosi, kuna wachezaji tutawapumzisha kesho,” amesema Matola.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER