Matola: Hatutaichukulia poa Coastal

Kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi Kuu, Kocha Msaidizi Seleman Matola amesema hatutaidharau Coastal Union kutokana na kutokuwa kwenye nafasi katika msimamo.

Matola amesema tunahitaji alama moja tu kesho ili tutangazwe mabingwa wa ligi wakati Coastal inahitaji alama tatu ili kujinusuru na janga la kushuka daraja kitu ambacho kinaufanya mchezo huo kuwa mgumu.

“Hatutaangalia matokeo ya mzunguko wa kwanza ambayo tuliwafunga mabao 7-0 bali tutaingia kucheza mechi mpya tukihitaji ushindi bila kujali kilichotokea, hivyo tutaingia kucheza mechi mpya.

“Sisi tunahitaji alama moja ili tutangazwe mabingwa na wao wanahitaji pointi tatu kujinusuru, kwa hiyo haiwezi kuwa mechi rahisi. Ukiachana na matokeo yao bado Coastal inacheza soka safi,” amesema Matola.

Matola amesema katika mchezo wa kesho kutakuwa na mabadiliko kidogo ya wachezaji kutokana kuwapumzisha baadhi na kuwapa nafasi wengine ambao hakupata mechi nyingi za kucheza.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER