Matola asisitiza mshikamano Simba

Kocha Msaidizi, Seleman Matola amewaomba Wanasimba kurejesha ushirikiano na kuendelea kuipa sapoti timu baada ya matokeo mabaya tuliyopata kwenye mchezo wetu uliopita.

Matola amesema hakuna Mwanasimba ambaye hakuumia na matokeo ya mchezo uliopita lakini huo ndio mpira tunapaswa kusahau na kusonga mbele.

Matola amesema ameongea na wachezaji na wamemuhakikishia katika mchezo wa kesho dhidi ya Namungo tutajitahidi kupata matokeo chanya.

“Kilichotokea kimetokea, tugange yajao. Huu ni mpira na matokeo haya huwa yanatokea. Kila mtu ameumia lakini kama ilivyo ‘slogan’ yetu ya ‘Nguvu Moja’ basi tuendelee kushikamana sababu tunayo nafasi ya ubingwa.

“Ninawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi Uwanja wa Uhuru kuja kuipa sapoti timu ninaamini tutapata ushindi,” amesema Matola.

Akizungumzia mchezo wenyewe Matola amesema “Namungo ni timu nzuri, haikuanza vizuri ligi lakini mechi mbili zilizopita wamefanya kwahiyo haitakuwa mechi rahisi lakini tumejipanga.”

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER