Mashujaa wetu watakaoikabili Azam FC Fainali Mapinduzi

Usiku wa leo kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Amaan Visiwani Zanzibar kucheza mechi ya Fainali ya Michuano ya Mapinduzi dhidi ya Azam FC.

Kocha Pablo Franco hajafanya mabadiliko yoyote ya kikosi kilichoanza dhidi ya Namungo katika mchezo wa nusu fainali.

Medie Kagere na Kibu Denis wataongoza mashambulizi wakipata msaada wa karibu kutoka kwa Rally Bwalya na Pape Sakho.

Kikosi kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Jonas Mkude (20), Kibu Denis (38), Sadio Kanoute (13), Medie Kagere (14), Rally Bwalya (8), Pape Sakho (17).

Wachezaji wa Akiba

Ally Salim (1), Israel Patrick (5),Pascal Wawa (6), David Udoh (33), Bernard Morrison (3), Mzamiru Yassin (19), John Bocco (22),

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER