Mashabiki wamuaga Bwalya kwa minoti

Mashabiki wa Simba wamemlaki kiungo mshambuliaji Rally Bwalya na kumtunza pesa baada ya mechi dhidi ya KMC
ikiwa ni sehemu ya kumuaga rasmi ambapo hiyo ilikuwa mechi yake mwisho akiwa na kikosi chetu.

Tukio hilo limetokea baada ya mechi hiyo kumalizika kwa ushindi wa mabao 3-1, ambapo Bwalya alizunguka uwanja mzima kuaga mashabiki akiwapungia mikono kama ishara ya kuwaaga huku wao wakimtunza pesa kuonyesha mapenzi yao.

Bwalya amewashukuru mashabiki, wachezaji na benchi la ufundi kwa ushirikiano mkubwa waliompa katika kipindi chote alichokuwa na klabu yetu na daima ataendelea kuwakumbuka huku akitutakia heri kuelekea msimu ujao wa ligi.

Hata hivyo, licha ya kumuaga Bwalya amesema anaweza kurudi kama Mungu atamjalia kwa kuwa kazi ya mpira ni mzunguko wa kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

“Nawashukuru sana mashabiki kwa upendo mkubwa walionionyesha, wamenipa thamani kubwa na najiona mwenye bahati kuwa na familia hii. Siku zote Simba itabaki kuwa moyoni mwangu,” amesema Bwalya.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER