Mashabiki 35,000 kuziona Simba, ASEC Mimosas Jumapili

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limeruhusu mashabiki 35,000 kuhudhuria mchezo wetu wa kwanza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa Jumapili saa 10 jioni, Februari 13 Uwanja wa Benjamin Mkapa.

CAF imetaka kufuatwa taratibu zote za kujikinga na ugonjwa wa corona kama kukaa kwa nafasi baina ya mtu na mtu, kuvaa barakoa na kunawa mikono kwa maji safi.

CAF imesisitiza taratibu hizo kufuatwa hivyo kila shabiki anapaswa kuchukua hatua na kumlinda mwenzake aliye karibu yake kwa muda wote wa mchezo.

Uongozi wa klabu umepanga kuhakikisha maandalizi yote yanakamilika na taratibu zote zinafuatwa huku ukiwataka mashabiki kununua tiketi mapema muda ukifika ili kuondoa usumbufu siku ya mchezo.

SHARE :
Facebook
Twitter

3 Responses

  1. kwa tuliyopitia simba mechi tatu za ugenini vipigo viwili na sare moja , yametutia unyonge sana. tUNAOMBA TUJIPANGE VIZURI TUJENGE TIMU, WACHEZAJI WATIWE MOYO/ ARI IONGEZEKE. SIMBA SPORTS CLUB DAIMA. NGUVU MOJA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER