Manula, Mzamiru watwanga zote Stars ikiichapa Uganda, Misri

Nyota wetu wawili mlinda mlango Aishi Manula na kiungo Mzamiru Yassin ni miongoni mwa wachezaji wa timu taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ waliocheza dakika zote 90 katika ushindi wa bao moja dhidi ya Uganda ‘The Cranes’.

Mchezo huo wa kufuzu fainali za Afrika (AFCON) umepigwa nchini Misri katika Uwanja wa Canal Suez mjini Ismailia huku Uganda wakiwa ndio wenyeji.

Manula na Mzamiru wakishirikiana na nyota wengine wa Stars wamepambana mpaka dakika ya mwisho kuhakikisha wanatetea bendera ya nchi na wamefanikiwa.

Mlinda mlango namba mbili Beno Kakolanya yeye hajapata nafasi ya kucheza lakini alikuwa kwenye benchi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER