Manula, Miquissone, Onyango, watinga fainali Mchezaji Bora wa Mwezi

Mlinda mlango Aishi Manula, kiungo mshambuliaji Luis Miquissone na mlinzi Joash Onyango wameingia fainali ya tuzo ya mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Machi inayodhaminiwa na Emirate Aluminium Profile (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month).

Kamati maalumu ya tuzo hizo, imepitisha wachezaji watano ambao wamefanya vizuri zaidi kwa mwezi husika na kuwachuja hadi kufikia watatu ambao wameingia fainali.

Wachezaji ambao waliingia tano bora ni Clatous Chama na Taddeo Lwanga pamoja na hao watatu waliongia fainali.

Mshindi wa tuzo hiyo atapatikana kupitia kura zitakazopigwa na mashabiki kupitia Website hii rasmi ya Klabu.

Tuzo hizo zilianza Februari ambapo Miquissone aliitwaa na kujishindia milioni moja kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium.

Zoezi la kupigiwa kura limeanza rasmi leo na litafungwa Machi 31, mwaka huu saa sita usiku ambapo utaratibu wa kuhesabu kura kisha kumtangaza mshindi utafanyika.

SHARE :
Facebook
Twitter

20 Responses

    1. Na Mungu kwakuwa sio mwanadamu basi ameshatusikia maombi yetu na kayajibu sawasawa, sifa na utukufu ni vyake hata milele yote hakuna astahiliye zaidi yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER