Manula arejea langoni Stars

Mlinda mlango wetu Aishi Manula, atasimama katika milingoti mitatu katika kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kitakachoshuka dimbani kuikabili Niger kwenye mchezo wa kufuzu fainali za AFCON zitazofanyika nchini Cameroon mwakani.

Manula alipata majeraha ya kuumia vidole vya viwili vya mikono wakati wa maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Mei 22.

Baada ya jeraha hilo Manula alikosa mchezo wa Nusu Fainali ya Azam Sports Federation (ASFC) dhidi ya Yanga na leo anarejea langoni baada ya takribani wiki mbili.

Nahodha wetu msaidizi Mohamed Hussein naye ameanza katika kikosi cha kwanza cha Stars huku Kibu Denis, Mzamiru Yassin na Kennedy Juma wakiwa benchi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER