Manula aenda Afrika Kusini kwa matibabu

Mlinda mlango namba moja Aishi Manula ameondoka nchini leo kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu ya nyama za paja.

Manula alipata majeraha katika mchezo wa Robo Fainali ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Ihefu FC uliopigwa Uwanja wa Azam Complex, Aprili 7.

Daktari wa timu, Edwin Kagabo ambaye ameongozana na Manula amesema mlinda mlango huyo atafanyiwa upasuaji ikiwa ni sehemu ya matibabu yake.

Kagabo amesema watafikia katika Jiji la Johannesburg na ndipo upasuaji na matibabu yake yatafanyika.

“Tunaondoka kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu ya mlinda mlango wetu Aishi. Matibabu yake yatahusisha upasuaji kwahiyo kuhusu atakuwa nje kwa muda gani itategemea na upasuaji huo,” amesema Dk. Kagabo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER