Mangungu: Mageti yatafunguliwa saa tisa Jumapili

Mwenyekiti wa klabu upande wa wanachama, Murtaza Mangungu amesema mageti ya Uwanja wa Benjamin Mkapa yatafunguliwa saa tisa alasiri katika mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates Jumapili.

Mangungu amesema mageti huwa yanafunguliwa mapema lakini kutokana na uwanja kuwa mashindano ya usomaji Quran siku hiyo muda umesogezwa mbele ili kuruhusu waumini wa kiislamu wote watoke.

Mangungu amewaomba mashabiki waendelee kununua tiketi kwa wingi ili kuujaza uwanja kwakua tumepewa fursa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuujaza uwanja.

“Mageti yatafunguliwa saa tisa alasiri siku ya mchezo kwa kuwa uwanja utakuwa na matumizi mengine ya usomaji wa Quran kwa hiyo usitoke nyumbani ukafikiri utaingia mapema,” amesema Mangungu.

Mwenyekiti Mangungu ameongeza kuwa wanaobeza jitihada zetu katika kuingiza timu nne kwenye michuano ya Afrika kwa mara ya pili mfululizo wana nongwa.

“Kwa miaka miwili tunaingiza timu nne kwenye michuano ya Afrika lakini watu wanajifanya hawaoni hizo tunaita nongwa,” amesema Mangungu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER