Mangungu awapokea mashabiki Ndola

Mwenyekiti wa klabu, Murtaza Mangungu amewapokea mashabiki waliosafiri kutoka jijini Dar es Salaam kuja Ndola, Zambia kuipa sapoti timu katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos utakaopigwa kesho.

Mashabiki hao ambao wamejaza mabasi mawili makubwa wameondoka Dar es Salaam Jumatano saa moja usiku na kufika hapa Ndola leo saa nne asubuhi.

Mangungu amewashukuru mashabiki hao kwa kujitoa kwao hali na mali kuja Zambia kuhakikisha timu inapata ushindi.

“Kwa niaba ya Uongozi wa klabu ya Simba, nawashukuru wote kwa kuja Zambia kuisapoti timu. Uongozi wa Simba unathamini mchango wenu na lengo letu ni kuhakikisha tunapata ushindi,” amesema Mangungu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER