Mambo matano muhimu kuelekea mchezo wetu dhidi ya ASEC Mimosas

Leo saa nne usiku kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Felix – Houphouet – Boigny kuikabili ASEC Mimosas katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Kuelekea mchezo huo tumekuwekea mambo matano muhimu kabla ya mtanange wenyewe kupigwa.

1. Tangu mwaka 2022 tumekutana mara tatu tukishinda moja ASEC pia wakishinda moja na kutoka sare moja.

2. Tumekutana kwenye hatua ya makundi kwa mara mbili ndani ya misimu miwili.

Msimu wa 2021/22 tulikutana katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika na msimu huu wa 2023/24 tumekutana tena kwenye makundi ya Ligi ya Mabingwa.

3. Machi 20, 2022 mlinda mlango Aishi Manula alidaka penati mbili dhidi ya ASEC ingawa tuliopoteza kwa mabao 3-0.

4. Nyota sita mlinda mlango Aishi Manula, Mohamed Hussein, Henock Inonga, Mzamiru Yassin, Kibu Denis na Clatous Chama walikuwepo nchini Ivory Coast mwezi uliopita walipokuwa wanashiriki michuano ya AFCON.

5. Mara ya mwisho tulipokutana na ASEC mechi ya ugenini tulicheza nchini Benin.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER