Makamu wa Rais wa Al Hilal atua Dar

Makamu wa Rais wa klabu ya Al Hilal, Mohamed Ibrahim amewasili jijini Dar es Salaam mchana huu tayari kushuhudia mchezo wa kirafiki utakaopigiwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni.

Rais Mohamed amepokelewa na Mkurugenzi wa Mashindano na Wanachama, Mzee Hamisi Kisiwa katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere na kupelekwa moja kwa moja hotelini.

Baada ya kutua Mh. Mohamed ameushukuru Uongozi wa klabu kwa kukubali kuipokea timu yake na anaamini maandalizi ya wiki moja waliopata ni mazuri ambayo yatawasaidia kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Tunaushukuru Uongozi wa Simba kwa kukubali kutupokea na kusaidia kambi yetu ya maandalizi yetu. Simba ni timu kubwa tunaamini mchezo wa leo utampa kocha mwanga kuelekea mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns.

“Hali ya hewa ya Sudan ni sawa na hapa jijini Dar es Salaam kwahiyo wachezaji wetu wamepata maandalizi mazuri ya utulivu,” amesema Mh. Mohamed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER