Makala awapa siku 60 wavamizi Mo Simba Arena

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala ameagiza watu waliovamia eneo letu la Uwanja wa Mo Simba Arena kuondoka ndani ya miezi miwili (siku 60) kuanzia leo.

Hatua hiyo ya uvamizi imesababisha kuchelewa kwa ujenzi wa uwanja wetu kupitia fedha zilizochangwa na mashabiki wetu.

Kutokana na hali hiyo, ametoa kauli hiyo ya kuwaondoa wavamizi hao na kuongeza kuwa eneo hilo tulipewa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete chini ya Mwenyekiti Hassan Dalali na tuna hati zote halali za serikali.

Makala ameongeza kuwa mmiliki wa eneo lazima uwe na hati ili utambulike na serikali lakini watu wamevamia eneo bila woga na kujenga hivyo wanatakiwa kuondoka kwa muda niliopa.

“Kuvamia eneo ni uhalifu kama uhalifu mwingine, hili ni eneo la Simba na walipewa na Rais mstaafu Dk. Kikwete, kwa hiyo waliovamia nawapa siku 60 kuanzia leo kuhakikisha wanaondoka.

“Leo ni Septemba 14 nitakuja Novemba 13 kuangalia zoezi hili limefikia wapi,” amesema Mh. Makala.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Klabu, Barbara Gonzalez amesema fedha yote zaidi ya milioni 150 iliyochangwa kwenye zoezi la nani zaidi zitatumika kufanikisha ujenzi huo.

Mwakilishi wa Mkandarasi Mega Woodcraft (T) Ldt Jonathan Kibona amesema vifaa vya vipo tayari na ujenzi utakamilika ndani ya miezi ndani ya miezi miwili na nusu.

“Zoezi lilichelewa sababu kulikuwa na uvamizi lakini baada ya maelekezo ya Mkuu wa Mkoa na vifaa vipo tayari ndani ya miezi miwili na nusu uzio madhubuti utakuwa tayari,” amesema Kibona.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER