Machampioni wa Mapinduzi kurejea Dar mchana

Mabingwa wa Michuano ya Mapinduzi 2022 watarejea jijini Dar es Salaam leo mchana kutoka Visiwani Zanzibar wakiwa na taji mkononi baada ya kukamilisha malengo.

Kikosi chetu usiku wa kuamkia leo kimetawazwa mabingwa wa michuano hiyo baada ya kuifunga Azam FC bao moja kwenye mchezo wa fainali.

Baada ya kuwasili Dar wachezaji watapewa mapumziko mafupi ya kwenda kuziona familia zao baada ya kupita wiki mbili.

Baada ya mapumziko hayo kikosi kitarejea tena mazoezini kujiandaa na mechi yetu ya Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Uwanja wa Sokoine, Jumatatu Januari 17.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER