Mabingwa DR Congo kujipima na Simba Queens

Mabingwa wa Ligi ya Wanawake nchini DR Congo Timu ya FCF Amani iliyopo nchini kwa ziara maalumu kesho itacheza mechi ya kirafiki na kikosi cha Timu ya Wanawake, JKT Queens katika Uwanja wa Mo Simba Arena saa mbili asubuhi.

FCF Amani imetua nchini leo alfajiri tayari kwa ziara hiyo ambayo lengo lake ni kuongeza ushirikiano na uhusiano bora pamoja kukiweka sawa kikosi chake.

Timu yetu ya Simba Queens inaendelea kupata mechi za kirafiki ikiwa ni maandalizi kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa Ligi (Serengeti Lite Women’s Premier) utakaoanza Desemba 23, mwaka huu.

Kikosi cha FCF Amani kitacheza mechi ya pili ya kirafiki Jumapili katika Uwanja wa Mo Simba Arena dhidi ya wenyeji wake Simba Queens saa mbili asubuhi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER