Maandalizi ya Mchezo dhidi ya Singida FG yanaendelea vizuri

Kocha Msaidizi Seleman Matola amesema maandalizi ya mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Singida Fountain Gate utakaopigwa kesho katika Uwanja wa New Amaan Complex yanaendelea vizuri.

Matola amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na hakuna yoyote ambaye tutamkosa kutokana na majeraha au kutumikia adhabu ya kadi.

Matola ameongeza kuwa itakuwa mechi ngumu hasa ukilinganisha Singida tumetoka kuifunga wiki iliyopita katika mchezo wa hatua ya makundi.

“Kikosi kipo tayari kwa mchezo, wachezaji wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo wa kesho. Tunaushukuru kuwa hakuna mchezaji ambaye tutamkosa kutokana nakuwa majeruhi au kutumikia adhabu,” amesema Matola.

Aidha Matola ameweka wazi kuwa winga mpya Ladack Chasambi anaweza kuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Singida kesho kwakuwa nae atakuwepo kwenye mazoezi ya mwisho ya maandalizi leo jioni.

“Ladack ni mchezaji mpya na yupo na kikosi hapa Zanzibar, tunategemea atakuwa sehemu ya kikosi katika mchezo wa kesho,” amesema Matola

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER