M-BET wadhamini wakuu Simba Queens

Kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya M-Bet imeingia mkataba wa miaka mitano na klabu yetu kwa ajili ya kuidhamini Timu ya Wanawake ya Simba Queens.

Mkataba huo utakuwa na thamani ya Sh bilioni moja ambapo kila mwaka Queens itakuwa inapokea kitita cha Sh miluoni 200.

Mtendaji Mkuu wa Klabu, Barbara Gonzalez amesema kwa sasa Queens ni bidhaa bora sokoni ndiyo maana imeanza kusimama yenyewe kusaini mkataba bila kutegemea mgongo wa timu ya wanawaume.

“Kama nilivyowahi kusema awali Simba Queens ni bidhaa bora, kwa miaka mitano tumekuwa tukifanya vizuri leo tumeingia katika historia na kuwa timu ya kwanza ya wanawake kuwa na wadhamini binafsi,” amesema Barbara.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet, Allen Mushi ameyaomba makampuni mengine kujitokeza kuwekeza kwa timu za wanawake kwa kuwa soka lake linazidi kupanda kila kukicha.

“Simba Queens inaendelea kufanya vizuri na inastahili kupata udhamini, sisi kama M-Bet tuliweka wazi nia ya kuwekeza kwenye soka tumeanza kwa wanaume sasa tumekuja huku kwa wanawake,” amesema Allen.

Queens itavaa jezi zenye nembo za M-Bet kuanzia kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo itafanyika nchini Morocco kuanzia Oktoba 30.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER