Lukula: Wachezaji wanapokea mafunzo vizuri

Kocha Mkuu Charles Lukula, amesema katika siku tatu tulizopata kujiandaa na mchezo wetu wa kesho wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns wachezaji wanashika vizuri mafunzo wanayopatiwa.

Lukula amesema kuelekea mchezo wa kesho maandalizi yamekamilika na hali za wachezaji ni nzuri tayari kupeperusha bendera ya Simba na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Lukula ameongeza kuwa mchezo utakuwa mgumu kwa kuwa tunakutana na mabingwa watetezi lakini hatutishiki na tutaingia uwanjani kutafuta ushindi ili tutinge fainali.

“Nafurahi kuona jinsi wachezaji wangu wanavyopokea mafunzo tunayowapa, kwa siku tatu tulizofanya mazoezi baada ya mchezo wa mwisho naona jinsi wanavyojituma,” amesema Lukula.

Kwa upande wake Mlinzi Wema Richard amesema ingawa Mamelodi ni timu nzuri yenye uzoefu kwenye michuano hii lakini hatutaingia kinyonge badala yake tutapambana hadi mwisho.

“Mamelodi ni timu bora, ina uzoefu na ndiyo mabingwa watetezi lakini sisi hatukufika hapa kwa bahati mbaya kwa hiyo tutapambana hadi mwisho kutafuta ushindi,” amesema Wema.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER