Lukula: Mechi na Yanga ni kama fainali, ni Derby ya makocha

Kocha Mkuu Charles Lukula, amesema mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite Women’s Premier League (SLWPL) dhidi ya Yanga Princess utakuwa kama fainali kutokana na upinzani mkubwa uliopo.

Lukula amesema mara zote mchezo wa Derby unakuwa mgumu na ili uwe bingwa lazima ukutane na timu bora kwa hiyo tupo tayari kwa mpambano wa kesho.

Lukula ameongeza kuwa mchezo wa kesho pia utakuwa Derby ya makocha kwa kuwa kocha wa Yanga, Sebastian Nkoma alitufundisha msimu uliopita na anawajua vizuri wachezaji wetu kwa hiyo tunategemea kupata upinzani mkubwa.

“Itakuwa mechi ngumu, hii Derby na siku zote Simba ikikutana na Yanga inakuwa kama fainali. Tunafahamu Yanga ni timu nzuri na ina kocha mzuri pia lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda,” amesema Lukula.

Naye Nahodha wa kikosi, Opa Clement amesema kwa upande wao wachezaji wamepata maandalizi mazuri na wapo tayari kufuata maelekezo ya walimu ili kupata ushindi.

“Sisi tupo tayari, tumepata maandalizi mazuri kutoka kwa walimu wetu na morali ipo juu na kila mmoja anatamani awepo kwenye kikosi ambacho kitaanza, tunaamini tutapata ushindi,” amesema Opa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER