Lukula: Mchezo dhidi ya JKT utakuwa mgumu

Kocha mkuu wa timu ya Wanawake ya Simba Queens, Charles Lukula ameweka wazi kuwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Serengeti Lite Women’s Premier League (SLWPL) dhidi ya JKT Queens utakuwa mgumu.

Lukula amesema tunakumbuka JKT walitufunga katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi lakini tumejiandaa kikamilifu kuhakikisha tunalipa kisasi.

Lukula ameongeza kuwa lengo letu ni kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu hivyo tunapaswa kukusanya alama tatu katika kila mchezo.

“Ni mchezo mgumu, walitufunga mchezo wa kwanza tunataka kwenda kulipa kisasi ingawa tunafahamu tutapata upinzani mkubwa.”

“Tumejipanga vizuri kuhakikisha tunakusanya pointi zaidi ili tuzidi kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wetu,” amesema Lukula.

Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu utapigwa kesho saa 10 jioni katika Uwanja wa Meja Genarali Isamuhyo uliopo Mbweni.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER