Lukula kocha mpya Simba Queens

Uongozi wa klabu umefikia makualiano na Charles Ayeikoh Lukula raia wa Uganda kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Wanawake ya Simba Queens kwa mkataba wa miaka miwili.

Kabla ya kujiunga na kikosi chetu Lukula alikuwa akikinoa kikosi cha SHE Corporates ambao ndiyo mabingwa wa Ligi Kuu nchini Uganda.

Lukula ana leseni A ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) ambayo inamuwezesha kukiongoza kikosi chetu kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo yatafanyika nchini Morocco Novemba mwaka huu.

Lukula anakumbukwa kwa kukiongoza kikosi cha SHE Corporates kufika fainali ya michuano ya CECAFA iliyofanyika hapa nchini Agosti mwaka huu na Queens tukaibuka na ushindi wa bao moja.

Miongoni mwa timu alizowahi kuzifundisha Lukula tangu mwaka 2016 ni Nyamityobora FC, Kirinya Jinja S.S.S FC, Uganda Cranes U23, MUBS FC na SHE Corporates.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER