Lukula: Hakuna mchezaji ambaye tutamkosa kesho dhidi ya Yanga

Kocha Mkuu wa Simba Queens, Charles Lukula amesema katika mchezo wa Derby wa kesho dhidi ya Yanga Princess hakuna mchezaji yoyote ambaye tutamkosa kwa sababu yoyote.

Lukula amesema maandalizi yamekamilika na wachezaji wapo kwenye hali nzuri tayari kupambana kwa ajili ya kuhakikisha pointi tatu zinapatikana hasa ukizingatia tutaingia tukiwa tunaongoza ligi.

Lukula ameendelea kusema kuwa siku zote mechi ya Derby inakuwa ngumu lakini kwa upande wetu hatutaki kupoteza alama yoyote sababu lengo letu ni kutetea ubingwa.

“Tunaenda kucheza mechi ya Derby kesho tukiwa tunaongoza hatutaki kupoteza alama yoyote kwakuwa lengo letu ni kuchukua ubingwa ili tupate nafasi ya kushiriki CECAFA na baadae Ligi ya Mabingwa Afrika.”

“Kama tunataka kuchukua ubingwa tunapaswa kushinda mechi kama hii, Ligi ya msimu huu ni ngumu ndio maana hata ukiangalia msimamo tofauti ya pointi tumeachana alama chache,” amesema Lukula.

Kwa upande wake nahodha wa kikosi, Mwanahamisi Omary amesema wamepata maandalizi mazuri na wapo tayari kwenda kufanya kazi ambayo wanatakiwa kuifanya kesho.

“Tumejiandaa vizuri kwa mchezo wa kesho, hii ni Derby kubwa, sisi wachezaji tupo tayari kufanya kazi ambayo tunatakiwa kuifanya ya kupambana kupata pointi tatu,” amesema Mwanahamisi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER